logo

NOW ON AIR

Listen in Live

(+Picha) Kizaazaa huku ajenti mkuu wa Raila akidai 'Bomas ni eneo la uhalifu'

Mawakala wa Azimio walidai kuwa kuna kasoro katika zoezi la uhakiki.

image
na SAMUEL MAINA

Uchaguzi13 August 2022 - 21:13

Muhtasari


  • •Mawakala wanaoshirikiana na muungano wa Azimio walikuwa wakidai kuwa kuna kasoro katika zoezi la uhakiki.
Maafisa zaidi wa polisi waliongezwa kwenye jumba hilo baada ya kamishna wa IEBC Abdi Guliye kuamuru watu wasio wa muhimu kutoka katika kituo cha kitaifa cha kuhesabia kura, Bomas of Kenya mnamo Agosti 13/

Hali ya mtafaruku imezuka tena katika ukumbi wa Bomas of Kenya na kusimamisha zoezi linaloendelea la uhakiki wa kura za urais.

Mawakala wanaoshirikiana na muungano wa Azimio walikuwa wakidai kuwa kuna kasoro katika zoezi la uhakiki.

Baadhi yao walidai kuwa baadhi ya maafisa wa IEBC walikuwa wakishirikiana na wapinzani wao kubadilisha matokeo na kunyakua fomu 34 A.

Mara moja, ajenti mkuu wa Raila Saitabao Ole Kanchory alitembea hadi jukwaa la VIP ambapo mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati na timu yake huketi, akanyakua kipaza sauti na kusema:

"Nataka kuwaambia Wakenya kwamba Bomas ni eneo la uhalifu."

Hadi wakati wa ripoti hii, zoezi la uhakiki wa kura lilikuwa limesimama.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved