Raila apendelewa zaidi kutwaa urais dhidi ya Ruto- Kura ya maoni

Raila anaongoza kwa asilimia 43 huku Naibu Rais William Ruto akiwa wa pili kwa asilimia 37.

Muhtasari

•Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Roots George Wajackoyah anachukua  nafasi ya tatu kwa asilimia 4.

Naibu rais William Ruto na kinara wa ODM Raila Odinga
Naibu rais William Ruto na kinara wa ODM Raila Odinga
Image: STAR

Mgombea urais wa Azimio la Umoja Raila Odinga anasalia kuwa mgombea anayependelewa zaidi, katika kura ya maoni ya hivi punde ya Infotrak.

Katika kura hiyo, Raila anaongoza kwa asilimia 43 huku Naibu Rais William Ruto akiwa wa pili kwa asilimia 37.

Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Roots George Wajackoyah anachukua  nafasi ya tatu kwa asilimia 4.

Kura hiyo ya maoni ilihusisha wahojiwa 9,000 kutoka katika maeneo bunge 290 kote nchini.

Mengine yanafuata...