Kwa sababu ya kipato chao kidogo ndoa yao haikuwa ya bonge la sherehe na mbwembwe ila baada ya wazazi wa pande zote kujulishwa na kutambulishana ,wapendanao walianza kuishi pamoja kama mke na mume .Kila kitu kikawa sawa kwa mwezi mmoja lakini katika moyo wake kuna uzito ambao ulimjia Alice akiwa katika boma la kina mumewe . Alishangaa mbona wanakijiji walimuangalia kwa huruma ni kana kwamba kuna jambo walilotaka kumwambia .Kila alipokwenda mtoni kuteka maji ,angekutana na wanawake wa kijiji wakiendelea pia na shughuli zake na baada ya kumsalimu wangemuuliza iwapo aliolewakatika boma Fulani .Alipojibu ndiye mke mpya katika boma hilo ,wengi walimuepuka na kuendelea na shughuli zao na alishangaa mbona .Hata hivyo kwa sababu ya ustaarabu alifikiri haingekuwa jambo la buara kumuuliza mume wake mambo kama hayo Ila hakujua yalimgonja !
‘USIWAHI KUOLEWA AU KUOA KATIKA BOMA LA WATU USIOWAJUA VIZURI.FANYA UCHUNGUZI USIJE UKAOLEWA KATIKA FAMILIA YA WEZI,WACHAWI NA KADHALIKA’ amesema Alice
Siku moja asubuhi mama mkwe alimwita Alice na kumfahamisha kwamba kuna wageni ambao watakuja jioni hiyo kwa hivyo afanye matayarisho la kufanya usafi na kufagia visehemu vilivyodondokwa na matawi na kasha atayarishe uji mzuri wa wimbi . Duh! Ilionekana kazi rahisi mtoto wa wenyewe akajua muda mfupi ujao atamaliza shughuli hiyo na awangoje wageni . Ilipotimu majira ya jioni , gsa likikaribia , Alice akaketi nje ya chumba chake akingoja basi wageni waje na alijua wataingia katika nyumba ya mama mkwe wake . Muda mfupi baadaye ,mama mkwe alimuambia alete uji ambao aliutayarisha auweke nje hapo karibu na nyumba yake kasha akae kando .Mgeni alikuwa njiani anakaribia kuja . Akashangaa mbona tena mgeni apewe uji akiwa nje ? Mbona tena wenyeji watangoja katika vibaraza vya nyumba zao wakimuangalia mgeni akinywa uji? Lakini muda haukumpa dakika za kuweza kupata majibu .
‘SIKUTAKA KUJUA KAMA NILIMPENDA MUME WANGU.THE FACT THAT KWAO KULIKUWA NA NYOKA NILISALIMU AMRI’ Alice anasema
Pembeni Alice alimsikia mama mkwe akijawa na jazba ya kiasili akiimba wimbo uliosikiza kama wa kitamadauni na kilichokuja karibu na sehemu ambapo uji uliwekwa ni Joka kubwa jeusi ambalo lilimfanya kaishiwa nguvu miguuni! Asijue la kufanya,maskini mtoto wa wenyewe alizirai. Wakati ‘mgeni’ alipokuwa akinywa uji, Alice alikuwa amepoteza fahamu !
‘SIKU HIZI WATU HUKUTANA KATIKA MIJI NA WANAANZA UHUSIANO BILA KUJALI KUHUSU HALI YA WENZAO WANAKOTOKA,FANYENI UCHUNGUZI KWANZA,HUFAI KUWA NA HARAKA KUINGIA KATIKA NDOA’ Alice anashauri
Baadaye usiku huo ,akiwa sasa amepata fahamu ,mume wake walimweleza kuhusu ‘utamaduni wao’ na Yule’mgeni’ aliyekuwa kunywa uji . Mumewe alimuambia Yule nyoka yupo kika kizazi chao na kwa hivyo wanamlinda nay eye pia anawalinda kama familia na ukoo . Kwa ufupi Alice aligundua familia ile ilikuwa ya wachawi wa kuroga kumtumia Yule nyoka .Mwanzoni ilionekana kama ndoto lakini mtoto wa wenyewe keshoye , hakuweza kufikiria hata kufungasha chochote chake, alitoroka alivyokuwa nakurejea kwao.Ndoa yake ilifikika tamati papo hapo na hajawahi kuangalia nyuma .Umeshawahi kuyasikia kama haya?