Akihojiwa katika kipindi cha BarTender kinachoruka kupitia runinga inayomilikiwa na Diamond, Kusaga amefunguka kuwa sio vizuri kushindanisha ukumbwa wa vyombo vya habari nchini humo.
https://www.instagram.com/p/B57wL1JpHi-/
"Naomba nikwambie kitu kimoja. Mimi ukichukulia fiesta niliyofanya, haijawaji kunipa faida kwa miaka yote unaweza ukakataa..." Allisema Kusaga.
Ikizingatiwa kuwa msanii Ali Kiba utumbuzia katika matamasha haya ya Clouds, Diamond ilibidi atoe kauli.
"Wenyewe wanasemaga BABA KASEMA...Jamani haka Kamsemo kuna sehemu kanaingiaga Utamu bwana...." Aliposti Mondi kwenye Insta.
Mastaa hawa wawili wamekuwa katika bifu huku mashabiki wao wakiwa katika makundi mbalimbali ya kuwaunga mkono.
Fiesta la Wasafi kwa mara nyingi limeshindanishwa na fiesta la runinga ya Clouds.