Uchungu wa mwana: Mama azua vurugu kortini kwa kumzaba mshukiwa kofi

unnamed
unnamed

Mahakama kuu ya Eldoret ilipatwa na mshangao baada ya mama mmoja kumzaba kofi mwanaume mmoja aliyedaiwa kuwa muuaji wa mtoto wa mama huyu.

''Wewe ndio umeua mtoto wangu na umenikasirisha sana,' 'Beatrice Wanyota alisema huku akimzaba kofi mshtakiwa.

Mshtakiwa, jina lake Mustafa alikuwa anaongozwa na maafisa wa polisi mpaka kwenye hospitali ya Moi Teaching Referral ili apimwe ugonjwa wa kichwa kabla ya kupewa kiapo na hakimu mkuu.

Mustafa mwenye umri wa miaka 31 ameshtakiwa kwa kosa la kutoa maisha ya Emma Wanyota binti mwenye umri wa miaka 26 tarehe 30 mwezi wa tisa.

Maiti ya Emma ilipatikana katika shamba moja la nyasi iliyo karibu na nyumba yao.

Amini usiamini, aliyemuua alifanya kitendo cha kinyama kweli kwani alikata miguu na mikono ya binti huyu.

Mamake marehemu alisema kuwa alikasirishwa na vile ambavyo kesi ile ilikawia sana kusikizwa na ndipo bwana Githinji akamueleza kuwa lazima sheria ifuatwe na sheria ni kuwa, lazima mshukiwa apimwe kuhakikisha kuwa hana akili punguani.

''Kila wakati nipangapo kuja kusikia kesi ya mtoto wangu huwa naambiwa kesi hiyo imehairishwa eti mpaka mshukiwa apimwe.'' Wanyota alisema.

''Lazima tufuate sheria, na sheria ni kuwa lazima mshukiwa apimwe akili kwanza kudhibitisha kuwa yeye si mgonjwa wa akili kabla ya kuhukumiwa.''Githinji alisema.

Mustafa pia ameshtakiwa kwa kosa la kumuua aliyekuwa mpenzi wake, Bi Nancy Etome tarehe 25 mwezi wa saba mtaa wa Uasin Gishu.