Ufisadi! Wakurugenzi wa Keroche wafikishwa kizimbani.

TABITHA.1 (1)
TABITHA.1 (1)
Wakurugenzi wa kampuni ya Keroche Tabitha Karanja na mumuwe Joseph Karanja wamefikishwa katika mahakama ya Milimani kujibu mashtaka ya ufisadi.

Wawili hao ambao walikamatwa Alhamisi baada ya kulala katika majengo ya kampuni hiyo hata hivyo walikanusha mashtaka yote kumi dhidi yao mbele ya hakimu mkuu Francis Andayi.

Tabitha Karanja wa Keroche atiwa mbaroni

Tabitha alikesha katika korokoro ya polisi baada ya kuandikisha taarifa katika idara ya DCI, mumuwe Joseph Karanja hata hivyo aliachiliwa kwa dhamana ya polisi kutokana na hali yake ya kiafya.

Wakurugenzi wa Keroche wanadaiwa kukwepa kulipa ushuru wa takriban shilingi bilioni 14 pesa za Kenya.

Katika taarifa siku ya Jumatano, Karanja alisema kampuni yake haijashiriki ukwepaji wowote wa ushuru na kuongeza kwamba haikua haki kwa kampuni ya Keroche “kuhujumiwa na kudhalilishwa”

Walisafirishwa kutoka Naivasha hadi makao makuu ya DCI mjini Nairobi kwa mahojiano zaidi punde tu baada ya kukamatwa.

Wanawakilishwa na wakili James Orengo.