Uganda kuwapima mawaziri wake wote kuhusiana na corona

mu7
mu7
Taifa la Uganda limeanza kuwapima mawaziri wake kuhusiana na virusi vya corona baada ya kubainika kuwa waziri mkuu wa taifa hilo alikuwa ameambukizwa. Kulingana na msemaji wa serikali wa taifa hilo, mawaziri hao wote watapimwa kwa wiki mbili kutokana na shughuli zao za kila siku.

Ameongezea kuwa baadhi ya wafanyakazi wa serikali 79 waliokuwa wameambukizwa na virusi hivyo wameruhusiwa kuondoka hospitalini baada ya kupata nafuu.

Mapema taarifa zimejiri kuwa waziri mkuu wa taifa hilo Ruhakana Rugunda amelazimika kujitenga kwa siku 14 baada ya kubainika kuwa alikuwa ameambukizwa virusi hivyo.

Kufikia sasa Uganda imesajili visa 557 vya maambukizi huku visa vya hivi karibuni vikiwa vilitokana na madereva wa masafa marefu.

 Shughuli za uchukuzi wa umaa zilirelejea wiki hili baada ya serikali kulegeza masharti yake.