Chama cha ODM kilichompa tiketi ya kwenda bungeni kimesema mbunge huyo aliaga dunia kwa sababu ya kansa ." Tumehuzunishwa na kifo cha mwanachama wetu na mbunge wa Msambweni Suleiman Dori mapema leo . Kansa ,imemchukua tena kiongozi aliyejitolea wa Kenya . kwa watu wa msambweni, kaunti ya Kwale na eneo zima la Pwani poleni sana," Chama hicho kimeandika katika ukurasa wake wa Twitter.
Dori aliaga dunia katika hospitali ya Aga Khan ambako alilazwa katia kitengo cha ICU. Mkurugenzi wa Mamlaka ya ustawi Pwani Mshenga Rugha alialisema Dori alianza kuugua Jumapili na kukimbizwa katika hospitali hiyo. Mbunge huyo mwenye umri wa miaka 42 alikuwa akihudumia muhula wake wa pili kama mbunge wa eneo bunge hilo kwa tiketi ya chama cha ODM .
Kiongozi wa ODM Raila Odinga na rais Uhuru kenyatta pia walituma risala zao za rambirambi kwa familia ya Dori .