uhuru

Uhuru aagiza kusitishwa kwa mikutano ya La Mada

Rais Uhuru Kenyatta ameagiza mawaziri kutoka kanda ya Mlima Kenya kusitisha mikutano yao ya usiku katika Hoteli ya La Mada.

uhuru
Wandani wa Naibu Rais William Ruto walikaribisha hatua hiyo ya rais na kumtaka awachukuliye hatua wale ambao wamekuwa wakihudhuria mikutano hiyo. Katika hatua ambayo inalenga kutuliza joto katika chama tawala cha Jubilee, Uhuru aliagiza kuwa mikutano yote ya serikali “ lazima ifanye chini ya taratibu zilizoko za utendakazi serikalini”.

5 wafariki katika ajali kwenye barabara ya Machakos-Wote

Rais anasemekana kuwaeleza mawaziri kufanyakazi chini ya kamati mbali mbali za baraza la mawaziri na kuhusisha viongozi waliochaghuliwa katika “kushughulikia maswala yote yanayohusiana na maendeleo”.
Agizo hilo, kulingana na duru katika chama cha Jubilee, linajiri baada ya mkutano baina ya rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto juma lililopita.

UHURUTO
“Swala hili lilikuwa ajenda yao kuu wiki iliyopita walipokutana katika Ikulu ya Rais. Jambo lililoibuka ni kwamba mkutano huo ulikuwa unavuruga serikali. Ilibidi wafanye uamuzi; utaona hatua zaidi zikichukuliwa dhidi ya maafisa wa hadhi ya juu katika serikali,” duru katika serikali ziliambia The Star.

Makampuni ya ubashiri yaongoza katika kuwekeza kwa matangazo ya biashara

Uhuru, pia inasemekana aliagiza mawaziri wote, makatibu wa kudumu na maafisa wakuu serikalini kufanya kazi kwa kuzingatia agizo la rais nambari moja la mwaka 2019 (Executive Order No. 1 of 2019) lilitolewa mwezi Januari.
Pia kuna kamati maalum ya kiufundi chini ya uwenyekiti wa katibu wa kudumu wa Usalama Karanja Kibicho, naibu wake akiwa mwenzake wa fedha Kamau Thugge.

Photo Credits: File

Read More:

Comments

comments