Uhuru afoka! ni mjinga asiyejua maana ya BBI

UHURU.BBI
UHURU.BBI
“Isome kwanza ripoti ya BBI kabla ya kuikashifu,” rais Uhuru Kenyatta amesema.

Akiongea wakati wa hafla ya kufuzu kwa mahafala katika chuo kikuu cha Kibabii siku ya Ijumaa, Uhuru alisema kuna baadhi ya viongozi wanaoshinda wakikashifu ripoti hiyo na ilhali hawajui kilicho katika ripoti hiyo.

"Hakuna haja ya matusi, kama kuna wale wanasema hawaitaki na hata hawajui nini iko ndani," Uhuru alisema.

Aliongeza : "Ni mjinga pekee atakayesema hakuma maswala au changamoto nchini zinazohitaji kushughulikiwa na suluhisho kupatikana."

Uhuru aliuliza wakenya kusoma kwa makini ripoti hiyo itakapotolewa.

“Tuchukuwe muda kusoma ripoti hiyo pamoja na tuone ni mambo yepi muhimu yanayoweza kuboresha taifa letu, liwe na umoja na kufanya taasisi zetu kujumuisha hisia za kila mmoja,” Uhuru alisema.

Matamshi yake kuhusu BBI yalijiri muda mfupi baada ya mwenyekiti wa jopo la BBI Seneta Yusuf Haji kutangaza kuwa ripoti hiyo itawasilishwa kwa rais Jumanne wiki ijayo.

Jopo hilo liliundwa mnamo Machi tarehe 9 mwaka uliyopita baada ya rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani Raila Odinga kuafikiana na kukubali kufanya kazi pamoja kwa lengo la kuunganisha taifa la Kenya.