Rais Uhuru Kenyatta amemhongera waziri mkuu mpya wa Japan Yoshihide Suga kufuatia kuchaguliwa kwake kama kiongozi mpya wa taifa hilo . Suga anaichukua nafasi ya Shinzo Abe ambaye anang’atuka madarakani kwa sababu ya kudhoofika kwa hali yake ya afya .
Katika ujumbe wake kwa Suga rais Uhuru Kenyatta amemtakia kila la heri na kumuahidi kujitolea kwa Kenya kuendeleza uhusiano wa muda mrefu katika ya Kenya na Japan .
Amesema anatarajia kujenga uhusiano wa karibu Zaidi na utawala wake na kuzidisha biashara kati ya Kenya na taifa hilo la bara Asia .
Wakati huo huo rais Kenyatta pia amemuaga waziri mkuu anayeondoka Shinzo Abe akimshukuru kwa kuwa kiongozi aliyetegemewa kuendeleza uhusiano kati ya Kenya na Japan .
Amesema kupitia Abe Kenya ilipata ,msaada wa kifedha kuweza kufanikisha miradi kadhaa ya miundo msingi katika sekta za ujenzi wa barabara ,kawi na eneo maalum la EPZ huko dogo Kundu katika kaunti ya Mombasa