Rais uhuru Kenyatta ametuma ujumbe wa kuifariji familia,jamaa na rafiki za Chief Inspector wa Police Pius Kipserem Cheboswony.
Cheboswony, aliyega dunia jumatatu katika ajali ya barabarani kwenye barabara ya Oljororok-Dundori Road huko nyandarua alikuwa akismamamia Ikulu ndogo ya Sagana ana alikuwa amehudumu katika huduma ya polisi kwa miaka 28 .Katika ujumbe wake rais amesema taifa limempoteza afisa wa usalama aliyekuwa wa kujituma na ambaye kujitolea kwake kulimfanya kupendwa na wenzake.
Rais amesema ameiombea familia ya marehemu ili wapate kufarijika baada ya msiba huo .