Uhuru amuomboleza mfanyibiashara John Murenga

Murenga
Murenga
Rais Uhuru Kenyatta ametuma risala za rambi rambi kumuomboleza  mfanyibiashara na mwandishi  John Murenga .

Murenga, mfanyikazi wa zamani wa serikali  alikuwa mwenyekiti wa  Chancery Wright Insurance Brokers,aliaga dunia jumane asubuhi

Amemuacha mjane   Magda Mugenda watoto wanne na wajukuu 10 pamoja  na kitukuu mmoja .

Katika ujumbe kwa familia ya Murenga rais Kenyatta amemtaja mwendazake kama  mtumishi wa serikali aliyekuwa na bidii  na aliyefaulu  kutoka utumishi wa umma hadi sekta ya kibinafasi  kwa njia iliyowapa wengi matumaini katika biashara na waliotaka kumuiga .

Rais pia alikitaja kitabu cha marehemu  Destined to Leave A Legacy, kama  raslimali kubwa sana kwa vizazi vijavyo vya wafanyibiashara .

Marehemu alisomea  Nyeri High School, Makerere University  na Oxford University.

Akiwa Makerere University, Murenga  alikuwa  mwanafunzi wa rais mstaafu  Mwai Kibaki  na badaye wakawa washirika katika biashara .