Uhuru anapaswa kuita kamati ya bunge,' Hisia za Wakenya baada ya usemi wa Oscar Sudi

Baada ya mbunge wa Kapsaret Oscar Sudi kutoa matamshi yake ya kumsuta rais Na familia wakenya wengi walitoa hisia tofauti kuhusu matamshi ya mbunge huyo.

Sudi alikuwa akizungumzia kukamatwa kwa mbunge wa Emurua Dikirr Johanna Ng’eno aliyekamatwa siku ya Jumatatu alasiri kuhusiana na madai ya kutoa matamshi ya chuki na kudhihaki rais Kenyatta.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa facebook Sudi alisema ya kwamba akina mama wote wanapaswa kupewa heshima.

Hii ni baada ya naibu rais Ruto kujitenga na matamshi ya Sudi na Johana Ng'eno.

"Kwa kutoa ufafanuzi hapa, si kumtusi mama ya mtu nilirudia kwamba mama yangu,mama Ngina na akina mama wote wanstahili kupewa heshima

Hata hivyo mwenzangu Johana Ng'eno alikamatwa kwa kutaja jina lake mama Ngina, hamna mama wa mtu ambaye ni muhimu kuliko wa mwingine 

Hayo ndio maoni yangu." Aliandika Sudi.

Ni ujumbe ambao uliibua hisia mseto na hata mjadala kwenye mitandao hiyo na hizi hapa baadhi ya hisia za wakenya;

: So now why was your good friend mentioning the president's mother. Where did she come in. She's not a politician.
 :Uhuru should simply call a parliamentary group meeting and cool down the ongoing temperatures,he is the party leader.
:Absolutely true, Uhuru is a Product of the same process as Sudi and everybody,mamake isn't special than all other mothers, Kenya Sio Mali yake!!
:Sudi Respect all mothers you say?Sudi keep off my mother too she deserves the respect that you expect to be accorded your mother, remember the several times you mentioned her in your political quest!