patanisho.2019

PATANISHO: Nilienda Kuwatch mpira kurudi nyumbani bibi amenuna hadi leo haongei

Bwana Ochieng alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Christine, akidai kuwa aliporudi nyumbani baada ya kwenda kutizama mechi, mkewe alikuwa amenuna na isitoshe hadi wa leo hazungumzi naye.

Patanisho: Nililala kwa sitting room baada ya mke wangu kugeuka kwa kitanda akaface upside down

 

“Ilikuwa ni Jumamosi na kawaida mimi hutoka kazini saa saba na nilimpigia simu nikamweleza kuwa nitachelewa kidogo, sasa hiyo siku nilirudi nyumbani mida ya saa kumi na moja. Nikaingia nikamsalimu na hakunijibu sasa sikushughulika naye na nikaenda ku watch mpira.

Kurudi sasa nikapata haongei, nikamuuliza nini mbaya akakataa kuniongelesha mpaka wa leo, ile kitu namuuliza yeye hunijibu na anaendelea kunyamaza. Shughuli zote anafanya lakini hataki kunizungumzia.” Alielezea bwana Odhiambo akidai kuwa haelewi chenye kinaendelea.

PATANISHO: Gidi ambia huyo mwanaume tupatane 2021 simtaki sahii

Alisisitiza kuwa hana mpango wa kando na anashangaa mbona mkewe hamuongeleshi kwani yeye humpa kila kitu hadi ATM ambayo hutoa pesa anapohitaji.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya mwaka mmoja na nusu na wamejaliwa mtoto mmoja.

Alipopigiwa simu, bi Christine alikubali kuwa wawili hao wamekosana.

“Ilikuwa Saturday na yeye hufanya kazi half day na sasa ikifika saa saba yeye huwa amefika. Kumpigia simu hashiki sasa mimi nikatulia tu, ilipofika 5 ivi nikiwa nimesimama kwa balcony naye anakuja nikamuona na msichana mwingine na nikarudi kwa nyumba nikanyamaza.

Sasa alirudi na akatoka na kudai ameenda kutizama mpira so mimi sikuongea, naye akaenda na akarudi saa tano usiku sikuzungumza kwani sikutaka maneno mengi. Yule msichana alikuwa mweupe mfupi.” Alijieleza bi Christine.

PATANISHO: Bwana yangu amekua kama makanga, anasonga na kila mwanamke

Pata uhondo kamili katika kanda ifuatayo.

 

Photo Credits: victor TKO imboto

Read More:

Comments

comments