Uhuru atofautiana na Ruto, atetea BBI na Raila Odinga

spixezi6ghody2sfs5cb17cd056404
spixezi6ghody2sfs5cb17cd056404
Rais Uhuru Kenyatta ametofautiana na naibu wake Ruto kuhusu malengo ya BBI.

Kenyatta ameweka wazi kuwa yeye hana azimio lolote la kusalia katika serikali baada ya uchaguzi wa mwaka wa 2022.

Aidha, Rais amesema kuwa makubaliano yake na Raila Odinga hayana misingi ya kugawana mamlaka.

Akizungumza katika uzinduzi wa reli ya kisasa hapa jijini Nairobi ,Nairobi Expressway, Uhuru amewataka wananchi kujiepusha na wanasiasa wanaoneza taarifa kuwa BBI inalenga siasa za 2022.

Maneno yake yamekinzana na ya Ruto ambaye alisema kuwa lengo la BBI ni kutengeneza viti wa watu wachache serikalini.

Tamko la wandani wa Ruto kuwa BBI inalenga kubadilisha katiba ili kutengeneza viti vingi katika serikali kuu linaonekana lilimfikia rais.

Nia na azma ya BBI ni kuwaleta wakenya wote pamoja na wala sio njama ya kugawa vyeo serikalini.

"BBI itatusaidia kufanya kazi pamoja, mimi na ndugu yangu Raila tutawaongoza Wakenya katika barabara hiyo ya kuungana..."

'BBI haiko kunipa kazi mimi, mimi nimechoka," alisema.

"Ni kuhakikisha kuwa Wakenya hawamwagi damu tena wakati wa uchaguzi, mtu asiwadanganye," Uhuru.

Ruto amekuwa mstari wa mbele kukashifu BBI hata kabla mapendekezo yatolewe.

Ruto amenukuliwa katika vyombo vya habari akitangaza kuwa mapendekezo ya BBI yatagonga ukuta kama ya Punguza mzigo ya Ekuru Aukot.