Uhuru azindua baluni za internet za loon ili kutumia vyema mtandao wa 4G

UHURU
UHURU
Rais Uhuru Kenyatta hatimaye amezindua kwa njia ya kidijitali baluni za internet za loon  ambazo  zitawawezesha watumaiji wa simu katika kaunti 14 kutumia mtandao wa 4G .

Hii ni baada ya kampuni ya Telkom Kenya kuingia katika makubaliano na  kampuni inayomiliki google  Alphabet  kwa kiasi kisichojulikana cha fedha  kuzitumia baluni maalum kuwezesha mawasiliano ya intenet  duniani.

Akizungumza  katika  kituo cha Radat Huko Baringo wakati wa uzinduzi huo kupitia  WhatsApp video, rais pia aliwahutubia  waliohudhuria hafla hiyo na kuwataka  waitumie vyema huduma hiyo na miundo misingi mingine iliyoboreshwa ya mawasiliano kudumisha shughuli za kiuchumi kuleta kipato.

"Sasa mna internet yenye kasi  zaidi na mtandao wa kutegemewa. Mnaweza sasa mkauza asali yenu kwa ulimwengu mzima, itumieni fursa hii vizuri’ rais amesema.

Waziri Wa ICT Joe Mucheru  ametaja uzinduzi huo kama wa kihistoria  akiongeza kwamba Kenya inazidi kuwa mstari wa mbele duniani kuhusu masuala ya teknolojia .