Uhuru Kenyatta azungumzia swala la Miguna Miguna kurejea nchini

Screenshot_from_2019_12_31_10_59_03__1577779165_84386
Screenshot_from_2019_12_31_10_59_03__1577779165_84386
Rais Uhuru Kenyatta amesema kuwa wakili Miguna ana uhuru wa kurejea nchini.

Aidha, rais amesema kuwa Miguna ana uhuru wa na haki zote za  kuzungumza ila anachokisema kiwe kinasaidia kuleta amani katika taifa la Kenya.

“Hakuna mtu ambaye amezuiwa kusema yale anayotaka kusema. Ata nasikia kuna wengine wanataka kupanda ndege warudi. Waendelee. Huo ni uhuru wao," alisema Kenyatta.

Hii ni baada ya Miguna kutangaza kurejea nchini mwezi ujao kupitia mitandao ya kijamii.

Katika mitandao ya kijamii, wakili huyu ambaye ana uraia tata alisema kuwa haogopi kusafiri nchini tarehe 11, Januari 2020.

Aidha, Miguna alichapisha nambari za dharura za kupiga iwapo kutatokea kizungumkuti katika safari yake.

Wakili huyu alifurushwa nchini mwaka jana baada ya tukio la kuapisha kinara wa chama cha ODM Raila Amollo Odinga.

"Hatutaita watu kuandamana. Huo utakua ujinga. Kihistoria, mageuzi na maendeleo ya kusonga mbele katika jamii husababishwa na thuluthi tatu ya watu. Kama hautaki mageuzi, tulia nyumbani. Wazalendo milioni 1 wataandaamana..." Alisema Miguna.