'Uhuru Kenyatta ni demokrasia,'Moses Kuria abadili tune

Mbunge wa Gatundu Moses Kuria Alhamisi alionekana kubadili ukosoaji wake, aliokuwa akimpa rais Uhuru Kenyatta ambaye alisifu kuwa ni demokrasia.

Moses Kuria alitoa maoni yake baada ya Uhuru kusema kuwa hatazidisha muda wake wa urais mnamo mwaka wa 2022 ukifika.

Mbunge huyo alisema kuwa Kenyatta ni demokrasia na atastaafu mwaka wa 2022 na ataendeleza kampeni za mwaka wa 2022 wakati wa uchaguzi mkuu.

"I have always maintained that Uhuru Kenyatta is a democrat. He will neither extend the term limit nor try to be Prime Minister. He will go home with grace and dignity in 2022. He will not support any candidate in 2022." Kuria Alisema.

Kwa miaka miwili sasa Kuria amekuwa akimkosoa rais Uhuru Kenyatta huku wakati mmoja akimwambia kuwa amerogwa.

Kenyatta aliahidi kuwa hataendeleza wakati wake wa kuwa rais wala hatawania kiti chochote, rais alisema kuwa anaheshimu katiba  na wala hakuzungumzia kuwa atawania kiti cha waziri mkuu.