Uhuru kumtumia DCI George Kinoti kupigana na Ruto - washiriki wa DP

Stephen Sang
Stephen Sang
Gavana wa kaunti ya Nadi Stephen Sang alimtuhumu rais Uhuru Kenyatta kwa kuungana na  kiongozi wa ODM Raila Odinga ili kufanikisha uadui wa kisiasa hasa kwa jamii ya Kalenjin.

Sang alimtuhumu Uhuru kumteua 'errand boy' Gearge Kinoti kuwa DCI kwa lengo fulani ya kunyanyasa jamii ya Kalenjin.

"Hatutakubali utumie Kinoti na DPP, kupigana vita vya kisiasa na tunaogopa unapeleka nchi katika mikono ya mbwa." Sang alisema.

Sang alisema kuwa wamepatwa na mshtuko mkubwa kwa sababu Uhuru anamuita Raila ndugu yake, ilhali uongozi wa ODM ulitenda kitendo cha uhaini kwa kumuapisha Raila kama rais wa watu baada ya uchaguzi uliopita.

Gavana huyo alisema kuwa Uhuru aache kufanya miradi ya kiwango cha chini eneo la Rift Valley na kukoma kunyanyasa watumishi wa umma wa jamii ya Kalenjin.

Aliongeza na kusema kuwa wafuasi wa Odinga walikuwa wanapayuka kila mahali wakisema kuwa nchi iko na rais wawili Uhuru na Odinga.

Sang na mbunge wa Kapseret Oscar Sudi walisema kuwa jamii ya Kalenjin iliweza kumuunga mkono rais Uhuru wakati wa uchaguzi kuliko jamii ingine yeyote ata wakati wa uchaguzi wa mwaka wa 2002 wakati hakuweza kuchaguliwa na wakikuyu.

Wakiongea maneno hayo wakiwa katika mazishi eneo la Ziwa kaunti ya Uasin Gishu.

"Kama wataka nafasi nyingine mwaka wa 2022, ongea nasi badala ya kutuuwa sisi sote ukisema kuwa wapigana na reshwa." Sang aliongea.

Sudi alisema kuwa Uhuru na Raila hawawezi kuwa kulelezo chema cha uadilifu kwa maana ata wao walikuwa wanafanya rushwa, akiongeza alisema kuwa wawili hao waache kusema viongozi wako katika sekta ya rushwa ilhali wao walikua hapo.

"Tutawaambia wananchi kuhusu kampuni zako zote na chochote ambacho tunajua kukuhusu, hauwezi kuwa unasema wale wengine ndio wezi na wewe ndio mwizi yule mkubwa." Sudi alisema.

Sudi alisema kuwa DCI George Kinoti angekuwa mkweli angekuwa ashaa wapata washukiwa wote wa rushwa.

"Kwa bahati mbaya Kinoti ni mchawi kama wale wengine, na hafanyi kazi kwa ukweli." Aliongea sudi.

Mbunge huyo alimlaumu Raila kwa kumpotosha rais Uhuru na kueza kumuacha naibu wake Ruto na jamii Kalenjin, alisema kuwa rais anapaswa kujitokeza na kuwaambia Kalenjin kosa ambalo wamefanya baada ya kumpigia kura uchaguzi uliopita.

Alisema pia kuwa raila ni mchawi na alimpea rais Uhuru dawa ya uchawi ili kumchanganya. Aliongeza na kusema kuwa kama rais alikosana na Ruto hapaswi kulipisha kwa jamii ya Kalenjin.