Uhuru kuwaambia mawaziri washirikiane na Matiang'i ama waache kazi

uhuru and CSs
uhuru and CSs
Rais Uhuru Kenyatta aliwaambia mawaziri washirikiane na katibu waziri wa mambo ya ndani Fred Matiang'i ama anayepinga mabadiliko kuwa waziri ni mkubwa wao aache kazi.

Pia aliwakumbusha mawaziri hao kuwa ni yeye tu pekee ana ruhusa ya kupeana mamlaka, na hatasita kuwalainisha wale ambao wataingililia ama kupinga agenda zake.

Januari 21 Uhuru aliteua (Four-tier executive authority) Matiang'i akiwa miongoni mwao na kuchaguliwa kuwa mkubwa wao.

Si mawaziri wote waliopendezwa na uamuzi wa Rais huku wakilalamika kwa yale Uhuru alifanya.

Muda mfupi baadaye, makamu wa rais Ruto aliweza kugeuka kuhusu kampeni zake za urais 2022, na kuelezea kuwa hajawahi jihusisha wala kufanya kampeni zozote baada ya uchaguzi uliopita wa 2017.

"Umefika wakati wa kusema mambo haya kwa makini kuwa kuna watu na vikundi ambao wanaenda wakini kampenia ."Alisema Ruto.

Jumanne, katika sekta ya mawaziri vita vilizuka baina ya mawaziri tano ambao wawili walimuunga mkono rais kwa uamuzi wake na watatu kujiunga na makamu wa rais wakisema kuwa kuchaguliwa kwa Matiang'i hakujatajwa katika sheria.

"Kama sheria, sisi sote ni sawa na sisi sote huwa tunafanya kazi sawa, itakuwaje mmoja wetu kutuandikia barua tumueleze kwa kifupi miradi ambayo tunafanya."Alieleza mmoja wa mawaziri.

Lakini rais Uhuru aliwaambia wazi mawaziri hao kuwa lengo lao kubwa ni kupeleka na kutoa huduma hasa katika agenda zake nne na si kufanya kampeni za uchaguzi wa 2022.

Mkutano huo wa jana ndio ulikuwa na mawaziri wote tangu Uhuru afanye mabadiliko.

Rais aliweza kuwaambia na kuwaeleza mawaziri hao kwa kina kuwa katika uteuzi huo wa mawaziri lazima kuwa na umoja na kuandaa kazi kulingana na ukabila hutakubaliwa katika sekta hiyo.

Inabaki kuona kama DP atasitisha kampeni zake za 2022 baadaya kushtumu  wazi wasaidizi wake.