Uhuru: Sikudhani uchaguzi wa Kibra ungekuwa wa amani

mARIGA IN KIBRA-compressed
mARIGA IN KIBRA-compressed
Rais Uhuru Kenyatta kwa mara ya kwanza amezungumzia kuhusu kushindwa kwa Jubilee katika uchaguzi mdogo wa Kibra.

Jubilee ilikuwa inampigia upato  McDonald Mariga katika uchaguzi huo uliowavutia wagombeaji 24.

Hata hivyo, Mariga alibwagwa na mgombea wa chama cha ODM.

Uhuru alikiri kwamba Jubilee ilishindwa ila akasema  cha muhimu ni amani uliodumishwa wakati wa kampeni na hata siku ya ukupigaji kura.

"Katika miaka yangu yote sijawai ona kampeni ya amani Kibra. Kuna baadhi ya watu wachache walirushiwa mawe lakini hatukuona duka likichomwa au watu wakiwa na wakati mgumu wakienda nyumbani," Uhuru alisema.

"Iwapo uchaguzi unaweza ukafanywa Kibra na watu hawatapoteza mali yao au maisha yao basi hiyo ni ushindi na watu wanafaa kujifunza kutokana na hilo,"

Alizungumza hayo katika ikulu ndogo ya Sagana katika kaunti ya Nyeri wakati alipofanya mkutano na wanasiasa kutoka Mlima Kenya.

Rais Uhuru alitoa mfano wa mfuasi wake ambaye kila wakati wa uchaguzi huvamiwa na kutpoteza mali.

Uhuru alisema kuwa kuna mwanamke aliyepotea mali yake katika uchaguzi wa 2007, 2013 na hata 2017 kutoka na vurugu zilizoshuhudiwa wakati wa uchaguzi.

Alisema kwamba kuwalika watu wengine kujumuik nao haimaanishi kwamba anawafukuza walio karibu na yeye.

Aidha aliwarai viongozi kutoka Mlima Kenya kusahau tofauti zao na kufanya kazi kwa pamoja.