Uhuru:Yaliyomo katika kapu la Shilingi Bilioni 53.7 za kuchochea ukuaji wa uchumi

Rais Uhuru Kenyatta ameratibu  programu ya hatua nane zitakazopokea  ufadhili wa serikali  ili kuchochea ukuaji wa uchumi  huku ulimwengu ukiendelea kupambana na janga la coronavirus .

Uhuru  amesema awamu ya kwanza ya mpango huo wa ufadhili  wa shilingi bilioni 53.7 utalenga miundo msingi .

Jumla ya shilingi bilioni 5  zitatengwa kusaidia katika kuwaajiri wafanyikazi  katika sekta mbali mbali ikiwemo ya afya .

Awamu ya pili itahusisha ufadhili katika sekta ya elimu .awamu hiyo inalenga kuhakikisha wanafunzi wanaendelea kupokea elimu kwa njia ya kidijitali na mifumo ya kisasa .

" serikali imetenga shilingi bilioni 6.5 kuwaajiri walimu 1000 wa mafunzi ya ICT kwa muda  ili kupiga jeki mpango wa masomo ya kidijitali’ amesema Uhuru

Mpango wa tatu utahusisha kupigwa jeki kwa biashara ndogo ndogo na za kadri  ambazo zimeathiriwa pakubwa na janga la corona .

Uhuru  amesema serikali imetenga shilingi bilioni 10  kulipa malipo ya VAT ambayo bado serikali inadaiwa na madeni mengine .

Awamu ya nne itakuwa kuwaajiri wafanyikazi 5000 wa afya ambao wana  Stashahada na Astashahad ambao watahudumu kwa kipindi cha mwaka mmoja .

Serikali inalenga pia kutoa shilingi bilioni 3 ili kuhakikisha kwamba wakulima wanapata  pembejeo  na kuwapa zuio la mahangaiko wakulima zaidi ya laki mbili wadogo wadogo .

Hatua nyingine zitahusisha shilingi bilioni 1  za kukabiliana na mafuriko ,shilingi milioni 540 za kupanda misitu , shilingi bilioni mbili za kukarabati  vivutio vya utalii na hoteli ,kuboresha uwezo wa Chuo cha Utalii , shilingi bilioni 1 za KWS kuwatumia maafisa wa kijamii katika utunzi wa mali asili na viutio vya utalii  na shilingi nyingine bilioni 1 za kuyatunza maeneo ya kijamii ya uhifadhi wa vivutio vya utalii .