Ujinga wa marais wa Afrika! Mutharika akataa kukubali kushindwa na mpinzani wake

PETER-MUTHARIKA
PETER-MUTHARIKA
Japo tume ya uchaguzi nchini Malawi MEC haijatoa wazi matokea ya uchaguzi mkuu uliofanyika katika taifa hilo ,taarifa zinasema kuwa rais wa sasa Peter Mutharika amekataa katia kukubali kushindwa na mpinzani wake wa karibu Lazarus Chakwera.

Mutharika amesema kuwa hakuna alishenda wala aliyepoteza na amekataa katakata kukubali kushindwa baada ya mahamaka ya taifa hilo kutoa agizo la kufanyika kwa uchaguzi mara ya pili kutokana na wizi wa kura ulioshuhudiwa awamu ya kwanza.

Kulingana na Atupele Muluzi ,ambaye alikuwa anawania kama naibu wa Mutharika ,amesema rais anawataka wafuasi wake wote kutupilia mbali matokea hayo akisema ni sharti matokeo halisi yatangazwe na tume ya uchaguzi ya MEC.

Atupele Muluzi ni mtoto wa zamani wa rais wa taifa hilo  Bakili Muluzi na kiongozi wa chama kidogo cha upinzani cha UDF ambacho kiliungana na chama cha Mutharika DPP.

Matokeo kutoka maeneo 28 yaliyotiwa sahihi na waangalizi wa uchaguzi huo pamoja na wawakilishi wa vyama yameonyesha kuwa Lazarus Chakwera amempigu Mutharika kwa umbali zaidi wa kura.

Chakwera ni kiongozi mkuu wa upinzani katika taifa hilo kwa chama cha Malawi Congress Party.