(+ Ujumbe) Diamond Platnumz kwa Prince Nillan, Zari akosa kumualika sherehe

Screenshot_from_2019_12_09_04_16_25__1575883073_13921
Screenshot_from_2019_12_09_04_16_25__1575883073_13921
Staa wa Bongo Diamond Platnumz amemtakia mtoto wake Nillan heri na fanaka katika sikukuu ya kuzaliwa kwake.

Katika mtandao wa Insta, Diamond Platnumz ameposti picha za Nillan na kuandika ujumbe kuwa anampenda zaidi.

Haya yanajiri huku staa huyu akikosa kualikwa na mama mzazi Zari The Boss Lady.

Nillan ni mtoto wa staa huyu na mwanamitindo kutoka nchi jirani ya Uganda.

https://www.instagram.com/p/B50QXmInz5T/

Uhusiano kati ya wazazi hawa wawili sio mzuri.

Wawili hawa walitemana baada ya tuhuma za usaliti katika ndoa.

Diamond amezaa na wanawanake watatu (Hamisa Mobeto, Zari The Boss Lady na Tanasha) .

Kuna kipindi na ambapo Diamond aliwahi kunung'unika kuwa hapewi nafasi nzuri ya kukaa na watoto.

Zari hakumwalika baba mtoto katika sherehe hii ya mtoto.

Diamond amewahi kukiri katika ngoma na kusema kuwa huwa anawaona watoto wake katika mtandao wa Insta.