Ujumbe wa Alex G Ndiritu wadhihaki baadhi ya Wananchi wa Amerika

Ujumbe wa mkenya na mkaazi wa kaunti ya Nyeri Alex G Nderitu wa kuwataka waandamanaji wanaoendelea kuandamana nchini Amerika kuchoma ikulu ya White House umepokelewa na baadhi ya wananchi wa taifa hilo kwa mshangao.

Nderitu aliyekuwa anafwatilia maandamano hayo kupitia kitandawazi cha Facebook aliwataka waaandamanaji kutekeleza tukio kama njia ya kilipisha kizasi kwa mwendazake George Floyd aliyeuwawa na polisi mzungu .

Ujumbe huo sasa umewafanya baadhi ya wananchi wa taifa kuzitaka asasi kuu za usalama kama vile CIA,FBI kuwa ange kwani huenda ujumbe huo ukawachochea waandamanaji hao kutekeleza kitendo hicho.

Muigizaji wa Amerika kwa jina Terence Williams kupitia ukurasa wake wa Twitter,ameitaka FBI na vitengo vingine kuwa macho.

“THEY ARE THREATENING TO BURN DOWN THE WHITE HOUSE! We must Protect President Trump and his Administration. All threats must be taken seriously. Please RT to inform the FBI, Secret Service and the CIA,” Terrence aliandika kwa Twitter.