Ukatili : Dada 2 wabakwa, na kuuawa kisii .

Watoto wawili wasichana ambao ni dada  walio na umri wa miaka sita na tisa  walibakwa jumatano usiku na kisha kuuawa katika eneo la   kaunti ya Kisii .

Ripoti zaarifu kuwa watoto hao walikuwa nyumbani pekee yao wakati wa tukio hilo kwa sababu mama yao alikuwa meenda sokoni .

Kamanda wa polisi wa kaunti ya Kisii Martin Kibet  amesema huenda watoto hao waliuawa baada ya kuwatambua waliotekeleza unyama huo . Visa vya ubakaji na wakati mwingine mauaji ya watoto vimekuwa vikiripotiwa kwa wingi katika sehemu mbali mbali za taifa .