Ukatili: Polisi Wanamsaka Jamaa Aliyedaiwa Kuwateka Nyara Na Kuwanajisi Watoto Wawili

Polisi jijini Kisumu wanamsaka jamaa mmoja anayedaiwa kuwateka nyara na kisha kuwadhulumu watoto wawili.

Mwathiriwa mmoja aliaga dunia, huku wa pili akiwa na majeraha ya unajisi.

Watoto hao wenye umri wa miaka 5 na 7 wanadaiwa kutoweka tarehe saba mwezi huu, baada ya kuchukuliwa shuleni na jamaa huyo kwa jina Habert Maliaka, katika shule ya Our Lady of Mercy eneo la Bandani jijini Kisumu.

Akidhibitisha kisa hicho, afisa mkuu wa trafiki eneo la Nyanza Andrew Naibei, amesema kua mtoto mmoja anaendelea kupokea matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga almaarufu Russia jijini Kisumu, huku mwili wa aliyefariki ukihifadhiwa katika hifadhi ya maiti hospitalini humo.

-Musa Naviye