Yaya mmoja huko Rongo amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani kwa kumbaka na kumwambukiza mvulana mwenye umri wa miaka 6 maradhi ya zinaa . Neema Matiko mwenye umri wa miaka 22 amepewa hukumu hiyo na hakimu mkuu wa Rongo Raymond Langat kwa kosa hilo alilotekeleza machi tarehe 30 mwaka huu .
Langat amesema amempa mtuhumiwa hukumu hiyo kali kwa kutumia vibaya maamaka yake kuhatarisha maisha ya mtoto huyo licha ya kufahamu kwamba alikuwa na maradhi ya zinaa .
Mtoto huyo amepewa matibabu ili kumzuia kuamubukizwa maradhi hayo . Akijitetea ,mtuhumiwa aliitaka mahakama kumwonea huruma kwa sababu kosa hilo lilikuwa lake la kwanza . Hakimu amesema ingawaje mtuhumiwa ana haki ya kujitetea ili ahurumiwe ,kosa lake ni kubwa kuliko sababu alizotoa ili kupewa msamaha .
Mtoto aliyebakwa , mamake na jirani ndio waliotoa ushahidi ddhidi ya yaya huyo huku ripoti kutoka afisa wa matibabu ikithibitisha kwamba kweli mtoto huyo alidhulumiwa kimapenzi .