Ajuza aliyebakwa na kisha kuuawa huko Nyahururu

UKATILI:Maajuza wa miaka 93 ,na 94 wabakwa na kuuawa Nyahururu na Kangundo

Umetendeka unyama huko Wiyumiririe, lokesheni ya Mutara ,Nyahururu  ambako ajuza mwenye umri wa miaka 93 alibakwa na kasha kuuawa . Mwili wa  mwathiriwa  Mukami Ndumia  ulipatika uchi  ukiwa  umefurika damu yake  jumatatu asubuhi katika tukio ambalo limewatamausha wenyeji . Polisi kutoka kituo kidogo cha  Ngobit wamemkamata mshukiwa mmoja kuhusiana na tukio hilo la kikatili.

UNYAMA!Jamaa ‘ambaka mbwa’ hadi kufa Kangundo.

  Kwingineko katika tukio kama hilo ,ajuza mwenye umri wa miaka 94 naye pia alibakwa na kasha kuuawa kwa kunyongwa katika  kijiji cha Kivaani,Kangundo .Kisa hicho cha Kangundo kimejiri wiki moja tu baada ya mwanamme mmoja katika eneo hilo kukamatwa na kufikishwa kortini kwa kufanya kitendo kisicho cha kawaida na mbwa hadi kumwua  mnyama huyo .

 BREAKING NEWS: MKASA: Watu 5 wa familia moja wafariki Mwatate

Photo Credits: Hisani

Read More:

Comments

comments