Ukistaajabu Ya Musa, Mbuzi Azaa Kimeme Kilicho Na Sura Ya Binadamu Kitui

Wakaazi wa kijiji cha Kangenge huko Kituo wameamkia mshangao leo  baada ya  mbuzi kuzaa kimeme chenye sehemu mbili; moja ya mbuzi na nyingine inayofanana na binadamu.

Wenyeji wamefurika katika kijiji hicho kushuhudia tukio hilo la kiajabu huku  uvumi ukizagaa kuhusu chanzo chanzo cha tukio hilo.

Baadhi wanadai kwamba huenda binadami alishiriki ngono na mbuzi huku wengine wakisema ni ishara ya ulimwenu kukaribia kufika tamati.