Ukitaka kurudi nyumbani ni sawa. Hiyo ni shauri yako! Rais Kenyatta

EcPOSWyXsAEM9cW.jfif
EcPOSWyXsAEM9cW.jfif
Rais Uhuru Kenyatta sasa amewataka wakenya kuwajibikia mienendo yao wenyewe baada ya kuondoa marufuku yaliyokuwa yamewekwa na serikali.

Uhuru Kenyatta: Kwa wale ambao watachukua fursa hii kwenda nyumbani, ujue jukumu ni lako kama wewe utawapelekea walioko mashambani ugonjwa…Kila mtu achukue jukumu lake

Akizungumza wakati wa hotuba yake kwa taifa, kiongozi wa taifa amesema  umefika wakati sasa ambapo wakenya wanastahili kujichunga kutokana na virusi vya corona ambavyo vimekuwa vikishuhudiwa nchini.

Stay safe, and recognise that the responsibility lies with you and me. - President Uhuru Kenyatta

Akitoa onyo kwa wakenya ambao watakuwa wakisafiri kutoka mjini kurejea nyumbani, Uhuru amesema ni jukumu la mtu kuhakikisha kuwa usalama wa familia yake uko sawa.

"It will not be the government's responsibility if those traveling spread the infection to their relatives upcountry"  Uhuru Kenyatta

Ameongezea kuwa serikali itakuwa macho ili kuangazia mienendo ya wananchi chini ya siku 21 kutathmini namna wakenya wanavyozingatia masharti yaliyowekwa na serikali.

President Uhuru: In the next 21 days we shall study the patterns of interactions and the spread of the disease.

Wakati uo huo, kiongozi wa taifa ametoa onyo kwa baadhi ya watu ambao hawaamini kuwa ugonjwa upo nchini akisema ni sharti kila mmoja awajibike awezavyo.

President Kenyatta: Serikali itachukua jukumu lake lakini ili tufaulu lazima kila mtu achukue jukumu kibinafsi…Tusidanganyane kuwa ugonjwa haupo..Ugonjwa upo… Hatuwezi kuwa na askari au wahudumu wa afya katika kila kanisa au msikiti…Viongozi wa kidini lazima wachukue jukumu