Screenshot_20200507-135900_Chrome-696x471

Uko na ujinga! Lulu Hassan amwambia Massawe Japanni baada ya kumpigia simu

Mtangazaji Massawe Japanni aliwapigia watangazaji Lulu Hassan na mumewe Rashid Abdalla katika kipindi chake cha bustani katika radio jambo.

Massawe alimpigia Rashid asubuhi na kumuuliza achague mtu mmoja ambaye angetaka kuongea naye wakati huo.

Rashid hakusita na alimchagua rais Uhuru Kenyatta ili aongee kuhusu janga la corona ambalo linahangaisha wakenya.

LULU 3

” Ningependa kuongea na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, kwa maana mimi ni mwanahabari ningetaka kuongea naye ili nimweleze  jinsi wanafanya kazi vizuri na mahali ambapo wamekosea.” Rashid Alisema.

Massawe alimshangaza Rashid kwa kumpigia mkewe Lulu badala ya rais Uhuru Kenyatta, kwa mara ya kwanza Lulu alikuwa anaongea na heshima lakini alicheka aliposikia sauti ya mumewe na na kumwambia Massawe,

“Uko na ujinga.” Lulu Alisema.

lulu hassan

Baada ya Rashid kuwekwa kwa laini alisema kuwa anataka kuongea na rais wa nyumba yake yaani Lulu.

Baadae Massawe alimuuliza Lulu nini hicho anataka kubadili katika maisha yake, naye Lulu alimuuliza mumewe ni nini ambacho hajawahi kupenda na angetaka kibadillishwe.

Kwa mengi zaidi sikiza mazungumzo yao kwenye mtandao;

https://www.instagram.com/tv/B_2xNkigr4O/?igshid=1dyig122e28fg

 

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO

Photo Credits: radiojambo

Read More:

Comments

comments