'Ukona mwaks?' na maneno mengine yatumikayo sana katika vyuo vikuu

chuo.kikuu
chuo.kikuu
Katika kila chuo kikuu humu nchini kuna maadili fulani ambayo hufuatwa na wanafunzi na ni maadili ambayo kila mwanafunzi wa chuo hicho anatambulika nayo.

Kisha kuna tamaduni ambazo huwa kwa takriban kila chuo kikuu ama ukipenda, kila mwanafunzi. Tamaduni hizi huletwa na tabia za wanafunzi na ili kuendeleza tamaduni hizi, aina ya lugha inayotumika huwa tofauti sana na lugha zingine.

Katika lugha hii ambayo ni mchanganiko wa lugha ya kimombo na swahili, kuna maneno ambayo huundwa ili kusaidia wanafunzi kuishi vyema na wenzao ama pia kuweza kuwa kwenye mstari wa kwanza kwa kila kinachofanyika chuoni.

Kwa mfano maneno haya ni kama "Uko na mwaks". Mhadhiri ni vigumu aweze kuelewa lugha hii kwani mwaks ni jina linalomaanisha mwakenya. Mwakenya ni kijikaratasi kidogo ambacho wengi huandikia majibu ya maswali na kubeba wakati wa mtihani.

Maneno mengine ni kama 'Pigwa exile'. Tofauti na udhaniavyo, hakuna aina ya vurugu yeyote inayoshuhudiwa hapa na kwani haya ni maneno yanayotumika na yeyote anaye fukuzwa kwa hostel endapo mwenzake amemkaribisha mpenziwe.

Kando na hayo, tumekuandalia orodha ya maneno 20 ambayo hutumika sana na wanafunzi wa vyuo vikuu. Jibambe!

1. Nitumie pdf

2. Nisignie attendance

3. Class/Cat imebounce

4. Class/Cat iko wapi

5. Pigwa exile

6. Supp inafanywa lini

7. Group yenu imejaa?

8. Uko na mwaks??

9. Ati uliniambia ii sem tunafanyanga unit ngapi

10. Password ya WiFi

11. Nipigie picha notes

12. Lec amefika?

13. Seconds before exam Them: niambie chenye unajua

14. Toa form ya mzinga

15. Next sem nitakua serious

16. Ina a group Nyi Fanyeni discussion me nitatoa pesa ya kuprint

17. *on Friday - uko wapi?

18. Tunatoa ngapi kila msee

19. Kuja sapa kwangu

20. Ongeza chwani tushike kaquorra