'Ulezi ni ngumu' Kambua azungumzia changamoto zake kama mama

Mwanamziki Kambua amekuwa mama kwa muda wa miezi mitatu na ni wazi kuwa huwa anajivunia sana kuwa mama.

Hata hivyo vile tujuavyo kuwa,hakuna kitu kilicho rahisi duniani. Kambua alifunguka na kueleza mwanzo mwisho maisha yake kama mama yako vipi.

Binti huyu alisema kuwa, pasi na kuwa amekosa usingizi siku nyingi na kufura macho na hata kuwa na uchafu mwingi kwenye nguo, hajuti hata kidogo kuwa mama kwani anajivunia sana kuitwa mama.

Aisee, kuzaa si kazi kulea ndio kazi.

          ''Eye bags. Burp on nearly all my clothes. Soiled diapers. Still, I wouldn’t trade this new adventure for  a anything. Motherhood is H.A.R.D! But oh so rewarding.''

Kambua alisema.Vilevile,Kambua alisema kuwa hata kama sazingine sisi huwaona kina mama wakiwanyonyesha watoto wao na tunafikiri kuwa ni kazi rahisi si kazi rahisi hata kidogo na kwa hivyo ikiwa amemuona mwanamke yeyote akiwa na matatizo,atakuwa wa kwanza kumsaidia mama huyu.

''Who knew that something as natural as breastfeeding could be so daunting? Or that sometimes your little one will cry and you’ll end up in tears yourself? Who knew that sleep could become such a luxury?🤷🏾‍♀️ I salute every mother who’s been on this journey. For staying on course amidst the challenges. And for not giving up. And to every new mummy like me, who’s navigating this path with a big L sign “kurutu”- you are doing just fine. You have all it takes to nurture that little one. And when you need to lean in and ask for help, please do! I’ll talk about my little village of helpers soon💛'' Kambua alisema.

Baada ya video ya Size 8 kuhusu mwendo wake wa kujifungua kitoto chake cha pili kusambaa kwenye mitandao ya kijamii,Kambua alimuandikia Size 8 ujumbe uliosoma,

“Today I celebrate Mama Wambo @size8reborn for crossing over victoriously! My own journey has taught me that it is nothing short of a miracle to conceive, carry, and birth a child. The journey was tough mama, but God carried you. We welcome your little one kwa shangwe na nderemo!!💃🏾🎉 Ah! Jehovah did it! You are dearly loved. May He pour more grace on you in this season 💛💛💛.” Kambua aliandika.

Ama kwa hakika,uchungu wa mwana aujuaye ni mama.