Ulianzia Ukambani kwa jina Colona,sasa Rayvanny aja na Corona!

NA NICKSON TOSI

Msanii wa nyimbo za kizazi kipya Rayvanny ametoa wimbo kuhusiana na virusi vya Corona ambavyo vimeathiri zaidi ya mataifa 123 ulimwenguni.

Katika wimbo huo Rayvanny anachukuwa fursa yake kuwaelimisha watanzania kuhusiana na jinsi ya kuzuiya virusi hivyo siku moja tu  baada ya kisa cha kwanza kuripotiwa nchini humo.

Rayvanny vile anamuomba Mwenyezi kuokoa ulimwengu dhidi ya virusi hivyo kutokana na idadi kubwa ya watu ambao ni maskini na hawana uwezo wa kukabiliana na virusi hivyo.

Rayvannya aidha alimshirikisha kiongozi wa Taifa John Pombe Mgufuli ambaye anasikika katika wimbo huo akitoa maelezo jinsi ya kuzuiya virusi hivyo.

Haya hapa ni maneno yake aliyoyasema katika wimbo huo wa Corona.

"Tanzania hatuwezi tukajiweka Pemebeni bila kuchukua hatua. Hatua zimeshaanza kuchukuliwa na waziri wa Afaya ameshatoa Tahadhari mbali mbali amabzo tunapaswa kuchukua. Napenda nirudie Ndugu zangu watanzania kwamba ni vizuri sana tukaendelea kuchukuwa tahadhari kwa nguvu zote. Ugonjwa huu unauwa na unaua haraka sana. Niwaombe Ndugu zangu watanzania tusipuzee ujongwa huu hata kidogo. Ni lazima tuanze kuchukua hatua za kujikinga na ujonjwa huu"Mugufuli anawasihi Watanzania katika wimbo huo.

Jumatatu wizara ya Afya ya Tanzania ilidhibitisha kisa cha kwanza cha Corona baada ya mwanhamke wa miaka 46 kuwasili kutoka Ubelgiji kufanyiwa vipimo vya matibabu na kupatikana na virusi hivyo.