''Ulikuwa umebobea sana kimuziki kabla ya kuoa.''Shabiki amuambia Daddy Owen

Daddy-Owen-kissing-his-wife
Daddy-Owen-kissing-his-wife

Daddy Owen ni mwanamziki wa nyimbo za injili ambaye alijifunga kibwebwe na kutia bidii sana ili kufaulu maishani kwani nafikiri alisadiki methali,mtaka cha mvunguni,sharti ainame.

Hata ikiwa Daddy Owen alikuwa na ndugu ambaye alikuwa ashafanya vyema kimuziki,Bwana Rufftone, ni wazi kuwa hakukata tamaa bali alizidi kutia bidii na kumcha Mungu.

Aisee mtegemea cha nduguye hufa maskini.

Mwanamziki huyu ndiye mwanamziki ambaye mpaka kwa sasa huimba nyimbo za injili.
Hata hivyo, kuna mashabiki ambao wanahisi kuwa,uimbaji wake umetokomea tangu afunge ndoa za maisha.

Shabiki mmoja bwana Fred Nixon ndiye aliyefunguka kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook na kusema kuwa,Daddy Owen alikuwaa mwanamziki wa nyimbo za injili amabye alimpenda sana kabla ya kuoa.
“Daddy Owen alikuwa anatesa industry vizuuuuri… alafu akaoa. Smh,” Nixon aliandika.
Hata hivyo, Daddy Owen alimjibu shabiki yule na kumwambia kuw, kuna wakati wa kila kitu.
''Oneni huyu sasa na kiherehere….hawa ndio wajuaji wa Nairobi ama? 🤣🤣🤣 anyway .. the Bible talks about seasons.. thrs time for everything my brother.''Daddy Owen alisema.

Owen Mwatia (Daddy Owen) alifunga pingu za maisha na mpenzi wake Farida Wambui mwaka wa 2016 na wamebarikiwa na mtoto mmoja wa kiume.

Wapenzi hawa walikutana kwenye mkahawa wa Java, wakabadilisha namba na wakaendelea na uhusiano wao kwa miaka minne kabla ya kufunga pingu za maisha.

Amini usiamini, hata ikiwa Daddy Owen ni 'Celebrity' ndoa yake na mke wake haijawahi kuwa na vioja .