Ulikuwa umetumwa na DPP kunitia kwa mtego? Mahojiano ya Babu Owino na mwanahabari Ann Kiguta yaenda mrama

Tjpk9kpTURBXy84YjZkYmVhODM5YWQ1YWMwMGU1MjIzMjVlM2ZiYzJiNy5qcGeRkwXNAxTNAbyBoTAB
Tjpk9kpTURBXy84YjZkYmVhODM5YWQ1YWMwMGU1MjIzMjVlM2ZiYzJiNy5qcGeRkwXNAxTNAbyBoTAB
Mahojiano yaliyokuwa yanasubiriwa kwa dhadi kati ya mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino na mwanahabari wa kituo cha K24 Ann Kiguta yalienda mrama baada ya wananchi waliokuwa wanafuatilia mahojiano hayo kutaka yakatizwe kutokana na kesi inayomwandama mbunge huyo.

Ifahamike vyema kuwa Babu Owino angali anakabiliwa na kesi ya kumpiga risasi mcheza santuri ama DJ Evolve ambaye hadi wa leo angali amelazwa hospitalini kutokana na majeraha mabaya ya shingoni aliyoyapata wakati wa tukio hilo.

Wakati mahojiano yalipoanza ,Kiguta alimuuliza wali kuhusiana na jumbe zake za kila mara mitandaoni akisema anawafunza wanafunzi wa kidato cha nne.

Na iwapo alikuwa anaitumia fursa hiyo kujitakasa dhidi ya shutuma zinazomwanadama kuhusiana na DJ  ,Babu alisema alianza kufunza akiwa shule ya msingi.

Kilele cha mahojiano hayo kilikuwa pale Kiguta alipoamua kucheza video ya Babu akimpiga risasi DJ katika klabu kimoja cha humu nchini.Babu aliamua kufunga domo na kukataa kata kulizungumzia swala hilo akidai kesi ilikuwa bado inaendelea kusikizwa mahakamani.

Baada ya kimya cha dakika kumi hivi ,Babu alihamaki na kudai huenda mwanahabari Kuguta alikuwa ametumwa na afisi ya mkuu wa mashtaka ya umma DPP ili kulizungumzia swala hilo na kumweka matatani.

"I think you were sent by the DPP to ask me these questions so that they can get an excuse for arresting me." Alizungumza Babu Owino.