Ulimwacha Tanasha kukimbilia mke wa Mtu?

kim.jfif
kim.jfif

NA NICKSON TOSI

Diamond Platinumz mpenziwe wa sasa Lilian Kessy almaarufu kama Kimnana amejaaliwa mtoto msichana na  kumuita Sky Tonny Albert kwa vile alipata ujauzito huo na mpenziwe wa kitambo Tonny Albert ,kabla ya kuanza kuchumbiana na Diamond.

Tonny Albert ambaye anadaiwa kuwa baba wa mtoto huyio aliandika haya.

'Sina mengi ya kuelezea namna ninavyo hisi kuhusiana na wanawake,nguvu na uwezo wao,uwezo wa kuwa tisti katika maisha pasi na changamoto ambazo wanapitia,natamani maisha kama hayo kila siku,wasichana wanaendesha ulimwengu,hiloo ndilo ninalofahamu kwa kwali,siku njema ya kusherehekea wanawake kwa mwanamke spesheli ambaye amenipa mtoto,nimefurahi kuwa baba'.aliandika Tonny.

Tonny aliongeza kuwa

'Shukran kwa wote mlionipongeza Mungu awabariki sana ,sina cha kuwapa ila tunawapenda'.alisema Tonny

Mwaka jana ,Kimnana ambaye alishirikishwa katika video ya wimbo wa Diamond ,alisemekana kuwa katika mahusiano na mhanyaji huyo baada ya kumulikwa katika maeneo tofauti ya burudani wakiwa pamoja.

Watumizi wa mitandao ya kijamii ni watu wa kushangaza sana na hawana ufahamu wowote wa kufuatilia ukweli wanaposikia uvumi kuhusu mtu,yale wanayoyajua ni kumuingilia mtu na kumdhihaki,nimeshangaa eti baadhi yao wangali wananihusisha na Diamond.kwa sasa mimi ninajishughulisha na maisha yangu ya kibinafsi.kama ningekuwa mpenziwe,tungekuwa tusha wafahamisha wafuasi wetu,alisema Kimnana.