Ulisema mkeo ni urembo tu!,Umerejea na Corona tena?

pjimage (13) (1)
pjimage (13) (1)

NA NICKSON TOSI

Msanii wa miziki ya injili Daddy Owen amejipata pabaya tena baada ya kusema eti vyombo vya habari vya humu nchini havijaweka mikakati yua kuwahasisha wakenya kuhusiana na virusi hatari vya Corona ambavyo vimetajwa kama janga kuu ulimwenguni na shirika la afya duniani (WHO).

Owen aliishtumu serikali kwa kukubali baadhi ya abiria kutoka mataifa ambayo yameathirika na ugonjwa huo kuingia nchini  akisema hakuna mipango mahsusi iliyowekwa kuthibiti maambukizi ya virusi hivyo ikiwa janga hilo litatufika.

Wakenya katika mitandao ya kijamii walionyesha hamaki zao na kumtaja kama mtu asiyejua  kusoma bali kuandika tu maswala ambayo yamekuwa yakitangazwa kila uchao na idara mbali mbali za serikali.

Vyombo vya habari vya Kenya vinaharakisha kuangazia tu maswala ya siasa pasi na kufahamisha umma kuhusiana na virusi vya Corona, vile tumejiandaa kama taifa ama wanangojea wakati kisa kimoja kitashuhudiwa nchini ndiposa waanze kuandika mabaya kuhusiana na maandalizi yetu.aliandika Daddy Owen

Bila kupoteza muda ,wakenya walianza kumrushia cheche za maneno katika mitandao ya kijamii, wakimtaja kama mtu asiyefuatilia kwa makini yale yanayoendelea nchini .

Haya ni baadhi ya maoni yao.

 kaka,tuna mengi ya kuzungumzia kama kuwaleta pamoja vijana katika sanaa zote ili kushirikiana na kufanya kazi pamoja.

 Wewe ni umaarufu tu unatafuta...vyombo vya habari vya humu nchini vimefanya uhamasishaji kuhusiana na mlipuko wa virusi vya Corona, juma moja lililopita, televisheni moja ya humu nchini iliandaa makala spesheli kuhusu virusi hivyo.

 Wamefanya kazi bora zaidi, anayesoma taarifa na kutazama katika televisheni anaona hayo.

 watu wamekuwa na hulka ya kutuandama sisi hata kama tunatekeleza kazi zetu vyema za kuelimisha wakenya .

Haya yanajiri siku chache tu baada ya msanii huyo kupayuka katika mtandao wake wa kijamii, siku chache tu baada ya orodha ya wasanii wanaolipwa vyema nchini kutolewa na kuandika katika ukurasa wake eti yeye ndiye akili na mkewe ni urembo, matamshi ambayo yalionekana na wengi kama ya kumdhalilisha mkewe.

Wengi walisema Owen alikuwa amekosea kuandika ujumbe wa aina hiyo, na kudai kuwa alimfananisha mkewe kama mtu aliyebarikiwa urembo tu na akili hana.

Je unadhani vyombo vya habari nchini havijafahamisha umma vya kutosha kuhusu virusi vya Corona?