Pesa za ukahaba ziliniwezesha kujenga Nyumba za ghorofa -Sarah

unnamed (8)
unnamed (8)
Sarah  Gitau  amekuwa akifanya kazi ya ukahaba kwa miaka 12 na hajutii uamuzi wake kwani anasema hali ya umaskini ndio iliyomfikisha  hatua ya  kuamua kuuza mwili wake lakini kamwe akitafakari muda wote huo hajutii lolote. Mbona hana majuto na ukahaba ni kazi ambayo wengi wana soni ya kujihusisha nayo?

Kwa muda wote huo akifanya ukahaba, Sarah ameweza kujenga nyumba mbili za ghorofa ambazo zina wapangaji na kila mwezi  analipwa kodi.

Ila mbona ilimchukua muda mrefu sana kuendelea na ukahaba endapo alifaulu kupata pesa  kutoka kwa nyumba zake za kupanga? Anasema ilifika wakati akazoaea kazi hiyo na licha ya kulipwa kodi, ilikuwa vigumu sana kuacha ukahaba hadi wakati  alipohisi kwamba kuna wanawake wa kisasa na wachanga  ambao walijitosa katika kazi hiyo.

‘Hakuna aliyejua kwamba nilikuwa nikifanya ukahaba Nairobi na hata kijijini  wengi walifikiri nilikuwa nafanya kazi ya kifahari’ anasema Sarah

Sarah anasema  kilichofanya pawepo na usiri kuhusu kazi yake ya ukahaba ni kwamba  biashara hiyo ilikuwa imejitangaza kama eneo maalum la kuwapa watu huduma za masaji. Wateja walikuwa wengi na hasa raia wa kigeni waliofurika eneo hilo ambako Sarah na wanawake wengine walikuwa wakija kufanya kazi hiyo.

‘Biashara yenyewe ilikuwa katika  mtaa mmoja wa kifahari  na eneo hilo lilikuwa limelindwa  sana. Hakuna asiyehitajika ambaye aliruhusiwa kuingia humo’

Sarah anasema aliambiwa kuhusu umuhimu wa kuanza kuwekeza akiwa yungali  ‘manyanga’ kwa sababu wakongwe katika kazi hiyo waliokuwepo walimsimulia jinsi wanawake ambao walikuwa wamefanya kazi sana katika eneo walivyoondoka bila chochote baada ya wateja kuwachukulia kama vikongwe na kuzipuuza huduma zao.

‘Hapo ndipo nilipoanza kujiwekea akiba na muda usiokuwa marefu nilinunua  ploti katika maeneo mbalimbali na kuanza kujenga’ anasema Sarah.

Kando na watu wa karibu wa familia, Sarah  anasema watu wengi hawajui kwamba ghorofa zake zilijengwa kupitia pesa alizopata kwa kufanya ukahaba.