Gavana Sonko amewahimiza wafuasi wake kusalia watulivu na kuachana na mpango wa kwenda katika mahakama ya milimani atakapofikishwa hapo kesho. Wakili wake Harrison Kinyanjui amesema Sonko hataki malumbano yoyote kati ya wafuasi wake na polisi kwani ana uhakika atathibitisha kwamba hana hatia .
Masaibu ya gavana Mike sonko yameonekana kuzidi kwani polisi sasa wanasema wanalenga kumshtaki kwa kumshambulia afisa mammoja wa polisi wakati alipokuwa akikamatwa huko Voi siku ya ijumaa. Charles Owino amesema sonko pia atakabiliwa na mashtaka ya kuharibu vifaa vya wanahabari, kukataa kukamatwa na kuwauzia polisi kutekeleza kazi yao.
Hayo yakiarifiwa, wakili Harrison Kinyajui anasema afisa wa polisi aliyenaswa katika video akimbeba juu kwa juu gavana wa Nairobi Mike Sonko wakati alipokuwa akikamatwa anafaa kukamatwa .Kinyanjui anasema Sonko anahitaji huduma za dharura za matibabu kwani aliumizwa wakati wa tukio hilo .
Hayo yakijiri, watu 26 wangali hawajulikani waliko na wanaminika kunaswa katika vifusi vya jengo liliporomoka mtaani Tassia siku ya ijumaa .maafisa wanaoendesha shughuli ya uokoaji wanasema idadi ya waliofariki bado ni watu watano huku 33 wakiokolewa na 18 wamelazwa katika hospitali ya mama lucy .