'Unamaanisha hana buruweein?' Mashabaki wamshambulia Daddy Owen kuhusu mkewe

daddy owen
daddy owen
Ilikuwa asubuhi safi sana kwa msanii Daddy Owen kabla ya kuamua kuchapisha picha yake na mkewe, Farida Wambui kwenye mtandao wake wa Instagram.

Picha haikuwa na shida hata! Na kama kawaida wawili hao wanapendeza zaidi ila kilichowasha moto ni caption yake kwani alisema,

BEAUTY and BRAINS

She's the Beauty and I am the Brains.

Caption hiyo haikuwafurahisha wengi haswa wanadada ambao walimshambulia Daddy Owen wakidai kuwa ni makosa sana kusingizia kuwa mkewe hana akili.

Rafikiye na mwanabiashara Chris Kirwa alitabiri kuwa kabla ifike jioni atakuwa amebadilisha caption na kuandika; Beauty and The Beast.

Hata hivyo kwa majibu yake, Daddy Owen hakushtushwa na maneno ya mashabiki wake ila alicheka tu na kulenga.

Soma baadhi ya jumbe zao,

2mbili: Broo unamaanisha hana buruwein, ama unataka ku cause pwein

Njeri: Wachana na Hawa wakuchungulia negativity from your caption..you are a great couple

MercyKaruru: Unamaanisha brain munatumia zako

Chris Kirwa: Kuna vile by jioni hii caption will change to Beauty and The Beast

Willis Raburu: So umeita bibi fala? Hahahahaha just kidding bro looking great 💯

Neeni: She is both gal power❤️

Joy: You're the head and she's beauty and brains😁....sidhani ye ni tail 😂🔥

Cate: You should've said the beauty behind my brains..Else you mean she's beautiful without brains  🤣🤣🤣