Unataka kuoa au kuolewa? Haya ndio unayofaa kujua

Kuna ongezeko la visa vya talaka katika ndoa na hata watu kuwa katika ndoa au mahusiano yenye vurugu na matatizo ya kuanzia  Timbuktu kdi Kabwodo Kingdom-matatizo mengi!  Chanzo wakati mwingi ni mtu kujiingiza katika ndoa bila kufahamu baadhi ya mambo .   Haya ndio unayofaa kujua kabla ya kujitosa katika kibarua cha ndoa

  1. Mwenzako hatokufanya kuwa mtu kamilifu

Kuna msemo kwamba mwenzako katika ndoa anakufanya uwe kamili,mstari huo mtamu kweli lakini endapo hutajua jinsi ya kujifanya mtu kamili kabla ya kuingia katika ndoa basi umejitayarisha kufeli .mwanzo unafaa kufahamu kwamba  kujua kujitunza wewe binafsi  ndio njia bora ya kujitayarisha kuweza kumtunza mwenzio kama wanandoa .Moja  na moja haziwezi kuwa mbili kama moja yenyewe sio kamili .

  1. Fahamu kuhusu matarajio unayokuja nayo katika ndoa

Una matarajio mwengi kwa mwenzio. Unataka mtu wa kukupakualia ngono kwa uzito kama  stadi.Unataka mtu atakayekuwepo ili usimezwe na upweke,unataka mtu ambaye atakuwa mzazi mzuri kwa watoto wenu  na hujajitayarisha kwamba mahaba kati yenu yatapungua baada ya muda . Yote makubwa lakini fahamu kwamba kuna matarajio ibuka ambayo yatakpa mshutuko wakati utakapotangamana na hali halisi ya kuishi pamoja kama mke na mume . wazungu kwa busara yao wanasema  ‘ There’s always a rude awakening when you first interact with reality’

  1. Hutajihisi kuwa katika ‘mapenzi’ wakati wote

Hisia za penzi ziko kama msimu ,uhusiano wako na mwenzako unafaa kuwa na msingi wa yote  mnayoamini  na bali sio tu kuhusu jinsi mnavyohisi . kuna siku ambazo utajihisi umejitenga au mwenzako hayupo katika mita bendi yako .wakati huo sasa ndio uaofaa kujua kwamba kuna mengi zaidi katika kupendana kuhusu hisia yenyewe ya mapenzi .

  1. Uhusiano mzuri na jamaa za mwenzio ni muhimu

Unafaa kujua kwamba kabla ya kukutana na mwenzako ,kuna watu  waliokuwa  nay kama wazazi ,ndugu na dadake zake na kadhalika ,utajenga uhusiano upi kati yako na jamaa zake wote.Hilo muhimu sana hasa iwapo utamuelewa mwenzake na hali zake bila kujifanyia maamuzi na kujenga dhana zisizowafaa . Maudhui katika familia zetu kujirudia au kuibuka tena katika ndoa zetu .

  1. Unafaa kujua hali ya kifedha ya mwenzio

Mnafaa kujua hali ya kila mmoja wenu kifedha ili kuweza kuamua jinsi mtakavyosimamia raslimali na matumizi yake .wengi siku hizi wanafahamika kuwa na  akaunti za pamoja za benki kisha kila mmoja kujitengea akaunti yake binafsi .  Ni njia nzuri kwa mujibu wa makubaliano yenu ,lakini swali linafaa kuwa ,mbona kila mmoja au mmoja wenu anataka kuwa na  akaunti yake? Je anahisi kwamba  anathibitiwa au anahisi kwamba amepoteza uhuru wake .Je,anahofu kwamba utamhadaa au  anahisi kwamba ni njia nzuri ya kuzidisha uhifadhi wa raslimali zenu ? majibu ya maswali hayo yatakuwa muhimu kufahamu ulipo uhusiano na ndoa yenu .

Inafahamika kwamba  suala  la pesa ni zito sana kwa wanandoa kulizungumzia hata kuliko kuzungumza kuhusu ngono

  1. Migogoro ni lazima-Tambua wajibu wako katika kuisuluhisha

Wakati uhusiano wenu unapoanza au ndoa ikiwa change ,huwezi kufikiria kwamba kutakuwa na malumbano na mwenzako . lakini yote hayo unafaa kufahamu yatategemea na jinsi wewe utakavyoyachukulia yakiibuka . Umejitayarishaje kuhusu wakati utakapogundua kwamba kuna tabia au vitu ambavyo huvipendi kwa mwenzio ?  jinsi ya kutatua  malumbano yote katika ndoa yenu au uhusiano yataibuka kwa ajili ya mtazamo wako na sio mwenzio .

Njia rahisi  ya kukabiliana na  hasira au mgogoro ni kufahamu kwamba yote yanaanza na wewe . Utawezaje  kuyakabili yote yanayotokea iwapo hujui jinsi ya kujithibiti au  kunyamaza? Watu wana wepesi wa kuchukua hatua na kufoka ,lakini watalaam wanasema cha muhimu ni kujipa muda wa kufikiria  na kusikiliza

  1. Jadiliana na mwenzako kuhusu athari za kuvunja uaminifu

Kuanzia mwanzo ,zungumzeni kuhusu muundo wa ndoa yenu.mtaaminiana nyinyi wawili tu au kila mmoja ataweza kuendelea na mahusiano yanayozuka na watu wengine ? usaliti utakuwa ni kwako ? Mwenzanko atakuwa ameipoteza  imani yako akifanya  kipi? Kuna wasiotaka wenzao watume jumbe za mapenzi  kwa watu walio nje ya ndoa yao,ilhali kuna ambao mambo yatavurugika endapo watagundua umelala na mtu mwingine nje ya ndoa .

  1. Mambo yanapokuwa magumu , msikimbilie kuvunja kila kitu kwa haraka

Vijana wengi wanatalakiana baada ya takribani miaka 5 katika ndoa . Kuna  dhana  siku hizi kwamba endapo mambo hayawaendei vizuri basi njia bora ni kukatiza papo hapo . Ila wasichojua wengi ni kwamba  migogoro katika ndoa au uhusiano  ni fursa  kwenu kuboreka .Iwapo tatizo sio dhulma kama vile kupigwa na mwenzio au mateso ya kifikra basi jipeni muda wa kunyoosha mkondo