Robert Burale

‘Unaweza enda Koinange kuuza mwili wako?’ Burale aongelea kuhusu ‘Sponsors’

Shinikizo la kudumu maisha ya kutamanika kwenye mtandao wa Instagram unazidi. Hali hii imewafanya vijana wengi haswa wanawake kuwa na mahusiano na wanaume wazee ambao wanagharamia mahitaji yao.

Wanaishi ni kama kesho haijathibitishwa na kauli yao ni ‘fake it till you make it.’

Katika kipindi kwenye chaneli ya Switch Tv, wanawake wachanga walikiri sababu zao kuwaona kimapenzi wanaume wenye umri mkubwa licha ya umri wao mdogo na sababu walizotoa ni za kustua.

Mmoja wa wasichana hawa alisema kuwa alipatana na mdhamini wake kwenye mtandao wa Instagram na yuko naye kwa sababu anahakikisha kuwa anaishi maisha ya juu sana na anaidumu.

Sponsor hataki nipate boyfriend na hanitoshelezi kitandani

Anasema,

”Sisi watu wachanga hatutafuti kuishi kwa furaha milele, wengi wetu tunatafuta msingi katika maisha yetu. Napendelea kuwa na mahusiano na wanaume wazee kuniliko. Wanaume wa umri sawa na yangu wana utoto sana. Nilipatana naye Instagram na tumekuwa pamoja naye kwa miezi sita na hadi sasa kila kitu ki shwari.”

Mwanamke mwingine aliongezea,

”Yote ni kuhusu kujenga jina lako katika mitando ya kijamii, naweza pata mwanaume ambaye ana umri mkubwa kuniliko ila nikose kumpenda lakini nitamtumia tu kupata pesa kutoka kwake.

Alitetea uamuzi wake kwa kukiri kuwa huwezi shinda ukiwaomba wazazi wako vitu ambavyo si mahitaji ya msingi.

Kusongwa nywele na kutengeneza kucha, huwezi waambia wazazi wako kuwa unataka kubadilisha mtindo wako wa nywele kila siku. Yote ni juu ya kujenga jina jema na njia  bora ya kutimiza hili ni kwa kutafuta mdhamini.”

Mchungaji Burale ambaye alikuwa kwenye jopo hilo hakuridhishwa na alijibu hivi:

”Ni haja gani uwe na mipango ya muda mrefu huku unahatarisha afya yako kiasi ya kuwa unaweza kosa kuishi muda mrefu sana kutimiza mipango yako? Kwa mwanadada aliyesema anawatumia tu wanaume, unaweza enda Koinange kuuza mwili wako?

Akihitimiza, Burale aongezea kuwa kumuona mtu kimapenzi aliye na umri zaidi sana kukuliko haina tofauti na ‘ukahaba’.

Hiyo ndiyo kitu haswa unafanya lakini kwa njia iliyo elimika. Wanadada walio Koinange pia huwatumia wanaume ili wapate pesa ya vitu mnazotaka nyinyi pia.”

 

‘Mimi sio mke wa jamii!’ Mwanasiasa Daisy Nyongesa awakanya shemeji zake

Burale aliwashauri,

Ni biashara moja lakini mazingira tofauti. Kitu moja ambayo nataka kukuhimiza ni kuwa, ikiwa unajijua ndani ya moyo wako nguo hazitakutambulisha. Utambulisho ni kuhusu jinsi ulivyo ndani ya moyo wako.

 

Photo Credits: Facebook

Read More:

Comments

comments