Undani wake A-Z Bob Collymore. Usichokifahamu kumhusu kipo hapa

BOB-COLLYMORE-FOOTBALL
BOB-COLLYMORE-FOOTBALL
Mtangazaji wa runinga ya Citizen Jeff Koinange amechora picha halisi ya Bob Collymore jinsi anavyoonekana katika undani wake ukiweka mbali maisha yake ya kazini na umaarufu.

Soma hadithi nyingine:

“Mapenzi ya shujaa huyu kwa wasiokuwa na uwezo wa kujisetiri kimaisha, huruma mwingi kwa waathiriwa wa majanga na matukio ya uhalifu, alivyojitolea katika uchapaji kazi na hatimaye wakfu wa Mpesa zilionyesha jinsi alivyojitahidi kutumia hela zake mfukoni kuwasaidia watu." alisimulia Jeff.

“Tukija kwenye kazi na wajibu wake kazini, alifanya kazi hiyo kwa kujitolea. Alielewa kuwa kweli ana pengo kubwa la kujaza na hangeweza kufanya masihara kamwe.Mimi siwezi kuijaza pengo la kiongozi huyu. Aliwahi kusema kuwa ataifanya kazi ya kuibadilisha Safaricom na kuitwaa katika levo za juu zaidi na ambapo wakosoaji wake hawatoweza kuamini."

"Ila kwetu sisi tungekutana mara kwa mara kikundi cha watu 5-7. Alikuwa mwenyewe Bob ama Kihara ama tu BC. Aliupenda muziki wa Jazz. Kuna kipindi angefinya uso ghafla akiona mapenzi yangu kwa muziki wa Country Music..." alieleza Jeff.

Soma hadithi nyingine:

Rafiki wa karibu wa Bob aliandika ujumbe huu kumhusu;

"Alijawa na furaha, nyemi kubwa zaidi akiwa huru na watoto wake, alitaka sana kuwasikiliza bila kujali umri wao. Aliishi maisha kwa ukamilifu na kwa sana aliipenda familia na taaluma yake."

Bob alipenda sana kusafiri, alikula na kunywa na wafalme na watu wa majina kubwa , marais na wakurugenzi na hatimaye kurudi nyumbani na kuabiri matatu akiwa na msanii Juliani na kuwatembelea wasiojiweza katika mitaa mabanda kama Huruma, Mathare, Mukuru and Majengo.