Under 18! Aliniambia ana umri wa miaka 23 kumbe alikuwa na miaka 17!

pjimage
pjimage
Wakati mwingi wanaume wanatahadharishwa kuwa makini wasije wakajipata mashakani kwa kujihusisha na watoto wlaio chini ya umri wa miaka 18 katika mambo   ya utu uzima . Siku hizi watoto wan miili mikubwa inayoweza kukudanganya kwamba ni watu wazima . Emmanuel Chule yuko  na kesi kortini kwa kupatwa na mtoto wa shule ambaye alimdanganya kuwa na umri wa miaka 23 lakini ukweli ni kwamba  ni mwanafunzi wa kidato cha nne aliye na umri wa miaka 17 .

Yote yalianza wakati walipokutana na katika eneo moja la Burudani  katika  huko Bamburi    Mombasa na wakabadilishana nambari za simu . wiki kadhaa badaye walikutana tena kwa chakula cha jioni katika mkahawa mmoja, Huku  Chule akikosa kufahamu kwamba alikuwa akitembea na mtoto wa shule . Mambo yake yalimwendea vibaya wakati  mmoja wa walimu wa msichana huyo alipowaona katika mkahawa huo na kumwita ili kumuuliza   mbona alikuwa  anatembea na mwanafunzi wake .

Chule alishangaa kwa sababu mtoto huyo wa skuli alikuwa amemhakikishia kwamba ametimu umri wa  kuwa mtu mzima n ahata akamuonyesha kitambulisho .  Baadaye  walipoendelea kuonana , kumbe mwalimu alikuwa amempigia simu  mamake  msichana huyo na kumshauri aripoti kwa polisi ili Chule akamatwe kwa ‘kumharibu’ msichana wa shule .

Chule alikuwa aktika utaratibu wa kujua ukweli iwapo msichana yule alikuwa na umri wa miaka 23 kama alivyodaiwa wakati maafisa wa DCI  pamoja na Chifu walipomkujia katika duka lake ka elektroniki mjini Mombasa na kumweka korokoroni kwa ‘kutembea’ na msichana wa shule .Ufichuzi baadaye umebaini kwamba msichana  yule alikuwa akitembea na kitambulisho  cha dadake na kwa sababu wanafanana hakuna aliyegundua kwamba  mtoto wa shuke alikuwa akijifanya kuwa dadake mkubwa .

Chule ameachiliwa huru kwa dhamana lakini kesi dhidi yak inaendelea hasa wakati huu ambapo mashirika mengi ya serikali yamejitolea kupambana na wanaume wanaofanya mapenzi na vitendo vya utu  uzima na wasichana wadogo . Ameendelea kujitetea kwamba hakujua umri wa msichana huyo wa shule ,lakini polisi na mahakama haijamuamini ingawaje kwa bahati nzuri amefaulu kuwashawishi wazazi kwa msichana yule kwamba hakuwa na nia ya kumharibu binti yao hasa baada ya  kudanganywa na kitambusho cha dadake mkubwa alichokuwa akikitumia kama chake .