''Unikome!Usiniletee mambo ya darasa la pili'.''Ali Kiba amuonya Diamond

diamond-kiba
diamond-kiba
Salaaale!Kitumbua kimeingia mchanga.
Mwanamziki stadi nchini Tanzania Ali Kiba amefunguka wazi wazi na kumuanika mwanamziki Diamond kwa sababu ya kuzungumza mengi kumhusu.
Kupitia mtandao wa kijamii, Ali Kiba alimuandikia Diamond ujumbe na kumtaka awache kufanya mambo kama mtoto wa darasa la pili.
” USINILETEE MAMBO YA DARASA LA PILI UNANIIBIA PENSELI ALAFU UNANISAIDIA KUTAFUTA .(UNIKOME). Ali Kiba alisema.

Ali Kiba aliongeza kuwa,

 ‘MWANAMUME HUONGEA MARA MOJA TU SASA UKITAKA NIKUWEKE UCHI WATU WAJUE UNAYONIFANYIA, HATA KWENYE HILO TAMASHA HATOKUJA MTU SASA TUISHIE HAPO NAKUTAKIA TAMASHA JEMA @DIAMONDPLATNUMZ

#KINGKIBA.

Inaonekana kuwa Ali Kiba anampa Diamond onyo awache kufanya mambo anayo fanya la sivyo atatoboa siri ambazo watu wengi hawafahamu.

Letu ni kukaa kitako kuona vita vya fahali hawa wawili vitafikia wapi.