Prof Stephen Kiama.

University of High Drama: Mahakama sasa yapuuza hatua ya Magoha kumtema Kiama kama VC wa UoN

 

Mahakama ya  ajira na Leba imetupilia mbali uamuzi wa waziri wa elimu George Magoha  kufutilia mbali uteuzi wa  Stephen Kiama kama Naibu Chansela mkuu wa Chuo Kikuu cha Nairobi . Jaji Maureen Onyango  pia amesitisha  kuteuliwa kwa  Profesa  Issac Mbeche  kama kaimu naibu chansela mkuu wa chuo hicho . Agizo hilo litasalia kuwepo hadi februari tarehe tani wakati  kesi hiyo itakaposikizwa .

DISARMED AND HOPLESS: Wafahamu Viongozi 7 watakaopokonywa ulinzi wa polisi na Bunduki .

Katika notisi aliyotuma siku ya jumapili waziri Magoha alisema mshikilizi wa kudumu wa wadhifa huo atateuliwa baada ya mashauriano. Lakini  aliongeza kwamba Kiama angeendelea kuhudumu katika wadhifa wake wa hapo awali kama naibu chansela anayesimamia wafanyikazi na utawala .

BATTLE FRONT :Jinsi Hatma ya Waititu inavyozua vita vya ndani kati Uhuru na Ruto .

Tangazo hilo lilitolewa baada ya Kiama kutuma mwaliko  kwa umma kwa hafla ya kukabidhiwa rasmi hatamu kama VC januari tarehe 21 . Badaye  mwaliko huo ulifutwa baada ya kuzuka vuta ni kuvute kuhusiana na usimamizi wa Chuo . Kiama ametuma taarifa akisema hatosalimisha majukumu yake kama mkuu wa taasisi hiyo licha ya agizo la Magoha

Photo Credits: Hisani

Read More:

Comments

comments