UNO ya Harmonize yatolewa YouTube, ubishi wa Magix Enga na Konde Gang

Meneja wa lebo ya Konde Gang ya Harmonize amefunguka kuhusu ngoma ya UNO kufungiwa.

Hii ni baada ya ubishi kuzuka kuwa midundo ya mkwaju huu ni ya producer wa hapa nchini Magix Enga.

Meneja wa Harmonize amefunguka kupitia mtandao maridhawa wa Insta,

"Tumepata taarifa kutoka mtandao wa YouTube kwamba producer wa Kenya ametuma baruapepe kudai umiliki wa ngoma ya UNO..."

https://www.instagram.com/p/B5FoMtwAdKK/

"Kwa utaratibu wa mtandao huu, ni lazima wafungie nyimbo hii kuonekana wakiendelea na juhudi za kufuata madai hayo..."

Meneja huyu aidha aliwaomba wafuasi na mashabiki wawe watulivu swala hili likifuatiliwa ili kubaini ukweli.

https://www.instagram.com/p/B5FVhVtHSS9/

Magix Enga ni producer mkubwa hapa nchini na alitoa lalama zake kuhusu midundo ya ngoma hii.

"1 Week Imeisha and The song Uno is no longer on YouTube Don’t sample magix Enga Beats. I repeat, dont! Like I said i’m not going to allow this to happen not in 254 🇰🇪.." Alichapisha Magix punde tu ngoma hiyo ilipofungiwa.